NYOTA wa zamani wa Cameroon, Samuel Eto'o amejiunga na klabu ya Sampdoria ya Italia kama mchezaji huru baada ya kuondoka Everton, imethibitishwa Jumamosi.
Kocha wa Sampdoria, Sinisa Mihajlovic alisema mapema kwamba Eto'o alikuwa anajiandaa kujiunga na klabu hiyo na akawaambia wachezaji wake wasishitushwe na ujio wa Mwanasoka huyo bora wa zamani Afrika.
Picha za Televisheni zimemuonyesha Eto'o, ambaye kwa sasa anachezea Everton, akiwasili katika kliniki mjini Rome kwa vipimo vya afya.Anatarajiwa kutambulishwa mbele ya umati wa mashabiki wa timu hiyo ya Jumapili katika mchezo dhidi ya Palermo.
Samuel Eto'o amejiunga na Sampdoria kama mchezaji huru baada ya kuondoka Everton
0 comments:
Post a Comment