MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto'o amekubali kujiunga na Sampdoria baada ya klabu hiyo ya Italia kufikia makubaliano na wakala wake.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 33 anayechezea Everton kwa sasa, amepewa ofa ya Mkataba wa miaka miwili na nusu na uwezekano wa kuwa kocha atakapostaafu soka.
Familia ya Eto'o bado inaishi mjini Milan na alikuwa anataka kurejea Italia.
Mshambuliaji Samuel Eto'o anajiandaa kuondoka Everton arejee Italia kujiunga na Sampdoria
Sampdoria inataka asafiri kwenda Genoa kesho tayari kwa vipimo vya afya Jumatatu kisha awekwe kwenye kikosi kitakachomenyana na klabu yake ya zamani, Inter Milan katika Kombe la Italia Jumatano.
Everton bado wanatafakari vipengele vya Mkataba wa uhamisho kabla ya hawajamkubalia kuondoka.
Kikosi cha Roberto Martinez kitamenyana na West Bromwich Albion Uwanja wa Goodison Park Jumatatu katika Ligi Kuu ya England.
0 comments:
Post a Comment