// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); DK FENELLA MGENI RASMI FAINALI KOMBE LA TAIFA WANAWAKE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE DK FENELLA MGENI RASMI FAINALI KOMBE LA TAIFA WANAWAKE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, January 30, 2015

    DK FENELLA MGENI RASMI FAINALI KOMBE LA TAIFA WANAWAKE

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Fainali ya Kombe la Taifa Wanawake Jumapili, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mechi hiyo itakayozikutanisha Pwani na Temeke itaanza Saa 8:00 mchana. 
    Temeke iliingia Fainali jana baada ya kuitandika Ilala mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, wakati Pwani iliifunga Kigoma 3-2.
    Waziri Dk Fenella Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasin katika Fainali ya Kombe la Taifa Wanawake Jumapili 

    Neema Paul alifunga mabao mawili ya Temeke katika mchezo huo, dakika ya 12 na 62, wakati mabao mengine yalifungwa na Shamim Hamisi dakika ya 69 na Stumai Abdallah dakika ya 70.
    Kipindi cha kwanza kilimalizika Pwani wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-1, ingawa Kigoma ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao. 
    Vene Gedion alianza kuwafungia Kigoma dakika ya 11 kabla ya Johari Shaaban kusawazisha dakika ya 15 na Amina Ramadhani kufunga la pili dakika ya 39.
    Kipindi cha pili, Pwani walirudi vizuri na kufanikiwa kupata bao la tatu kupitia kwa Tumaini Michael dakika ya 57, kabla ya Nahodha wao, Wema Richard kujifunga dakika ya 66 kuipatia kigoma bao la pili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DK FENELLA MGENI RASMI FAINALI KOMBE LA TAIFA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top