KOCHA wa zamani wa Manchester United, David Moyes usiku huu ameiongoza timu yake mpya, Real Sociedad kuiangusha Barcelona kwa bao 1-0 katika La Liga Uwanja wa Aneota.
Barcelona imepoteza nafasi nzuri ya kupanda kileleni mwa La Liga kwa kipigo hicho na kocha Luis Enrique atajilaumu kwa kuwaanzishia benchi wachezaji wake nyota wakiwemo Lionel Messi, Neymar na Gerard Pique.
Ushindi huo wa kikosi cha David Moyes ni muendelezo wa ubabe dhidi ya vigogo, baada ya awali kuwafunga Real Madrid na Atletico Madrid Uwanja wa Anoeta msimu huu.
Beki wa Barca, Jordi Alba alijifunga mapema dakika ya pili tu kuipatia ushindi huo timu ya Moyes. Mapema katika mchezo uliotangulia, Real Madrid ilifungwa mabao 2-1 na Valencia Uwanja wa Mestalla, licha ya Cristiano Ronaldo kutangulia kufunga.
Kikosi cha Real Sociedad kilikuwa; C. Martinez, Ansotegi, I. Martinez, De La Bella, Markel, Granero, Xabi Prieto, Canales, Castro/Finnbogason na Vela.
Barcelona; Bravo, Montoya, Mascherano, Mathieu/Alves, Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Munir/Messi, Suarez na Pedro/Neymar.
Luis Suarez (kushoto) akiwaangalia wachezaji wa Real Sociedad wakishangilia bao lao la mapema lililodumu hadi mwisho mwa mchezo huo wa La Liga
Kocha David Moyes akiwa kazini Uwanja wa Anoeta dhidi ya Barca
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2896419/Real-Sociedad-1-0-Barcelona-David-Moyes-giant-killers-prevent-Lionel-Messi-taking-spot-La-Liga.html#ixzz3NtTuNopf
0 comments:
Post a Comment