MUSTAKABALI wa kipa David de Gea katika klabu ya Manchester United upo shakani kwa sasa, baada ya jana wakala wake kushindwa kuwakatalia Real Madrid mpango wa kumsajili.
De Gea amebakiza miezi 18 katika Mkataba wake Old Trafford na bado hajakubali vipengele vya mkataba mpya, huku Real ikimfuatilia kwa karibu.
Wakala wake, Jorge Mendes, ambaye pia anamuwakilisha Cristiano Ronaldo, alipoulizwa na vyombo vya habari Hispania kama kipa huyo mwenye umri wa miaka 24 atahamia Madrid, alisema inawezekana.
"David na babu kubwa, ni kifaa," Wakala huyo Mreno amesema akizungumza na gazeti la Marca. "Ni mchezaji wa Man United na ana Mkataba kule. Unatakiwa kuheshimu hilo, lakini mambo yanabadilika kila dakika tano,".
Licha ya kumsajii kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes, kocha wa United, Louis van Gaal amesistiza kwamba De Gea atarefusha Mkataba wake wa sasa Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment