KLABU ya Chelsea imekubali kumuuza Andre Schurrle ili kupata fedha za kumnunua Juan Cuadrado.
Uhamisho wa Mcolombia, Cuadrado, mwenye umri wa miaka 26, unaweza kukamilika ndani ya muda mzuri ili aweze kucheza Jumamosi mchezo wa kuwania usukani wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester City, huku Chelsea ikikaribia kabisa kumsajili.
Chelsea imetaka zaidi ya Pauni Milioni 30 kumuuza Schurrie na Wolfsburg inaelekea kufika bei, huku Borussia Dortmund pia wakimuhitaji.
Jose Mourinho si mpenzi wa mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani, lakini anakiri ni wa thamani ya juu. Mshindi huyo wa Kombe la Dunia pia anataka kurejea nyumbani kwao.
Andre Schurrle yuko njiani kuondoka Chelsea baada ya klabu hiyo kukubali kumuuza
Cuadrado anaweza kusajiliwa ndani ya muda ili awahi mechi dhidi ya Manchester City Uwanja wa Stamford Bridge Jumamosi
0 comments:
Post a Comment