CHELSEA imezinduka na kuichapa maao 5-0 Swansea City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa leo, Uwanja wa Liberty.
Kiungo Mbrazil Oscar alifungua biashara kwa bao zuri dakika ya kwanza, kabla ya Diego Costa kufunga la pili dakika ya 20 na la tatu dakika ya 34.
Oscar akafunga tena dakika ya 36 kabla ya nyota wa Ujerumani, Andre Schurrle kukamilisha shangwe za mabao dakika ya 79.
Kwa ushindi huo, The Blues ya Jose Mourinho inafikisha pointi 52 baada ya mechi 22 na kujiimarisha kileleni, dhidi ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 47 za mechi 21.
Kikosi cha Swansea City kilikuwa; Fabianski, Tiendalli, Fernandez, Williams, Taylor, Dyer/Barrow dk74, Carroll, Sigurdsson, Routledge/Emnes dk32, Oliveira/Fulton dk66 na Gomis.
Chelsea; Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Luis, Matic, Fabregas/Ramires dk74, Willian/Schurrle dk76, Oscar, Hazard na Costa/Remy dk74.
Wachezaji wa Chelsea wakipongezana kwa ushindi wa leo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2914549/Swansea-City-0-5-Chelsea-Blues-boys-Brazil-batter-Swans-Jose-Mourinho-s-five-points-clear-table.html#ixzz3P6WsDMAl
0 comments:
Post a Comment