SAFARINI kuelekea Wembley. Habari ndiyo hiyo. Bao pekee la beki Branislav Ivanovic dakika ya 94 limeipeleka Chelsea Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup baada ya kuilaza Liverpool 1-0 Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Chelsea inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1, baada ya awali kutoa sare ya 1-1 Uwanja wa Anfield na sasa itamenyana na Sheffield United au Tottenham katika fainali Uwanja wa Wembley.
Diego Costa aligombana na Martin Skrtel katika matukio tofauti wakati wa mchezo huo Stamford Bridge na mashambuliaji huyo wa Hispania alionekana mwenye bahati baada ya kugombana pia na Emre Can na Steven Gerrard, lakini hakulimwa kadi nyekundu.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Zouma, Terry, Luis/Azpilicueta dk78, Fabregas/Ramires dk50, Matic, Willian/Drogba dk119, Oscar, Hazard na Costa.
Liverpool; Mignolet, Can, Skrtel, Sakho/Johnson dk57, Markovic/Balotelli dk70, Henderson, Lucas, Moreno/Lambert dk105, Coutinho, Gerrard na Sterling.
Wachezaji wa Chelsea Eden Hazard, Oscar na Branislav Ivanovic wakiwa wameshika bango la tunaelekea Wembley
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2928916/Chelsea-1-0-Liverpool-AET-agg-2-1-Branislav-Ivanovic-heads-Blues-Capital-One-Cup-final.html#ixzz3Q7HSnqAr
0 comments:
Post a Comment