KLABU ya Chelsea itamkosa mkali wake wa mabao Diego Costa kesho katika mechi ya kuwania usukani wa Ligi Kuu ya England, dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City baada ya kufungiwa mechi tatu na Chama cha Soka (FA).
Mshambuliaji huyo Hispania alikutwa na hatia ya kumkanyaga makusudi mchezaji wa Liverpool, Emre Can katika mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup Uwanja wa Stamford Bridge mapema wiki hii.
Costa alishitakiwa na FA Jumatano jioni na pamoja na utetezi wa Chelsea kwamba alikuwa haoni anapokanyaga mguu wake akamkanyaga kwa bahati mbaya Can, lakini ameadhibiwa.
Diego Costa, akiwa mazoezini na Chelsea jana, amefungiwa na FA kwa kumkanyaga Emre Can
Mshambuliaji wa Chelsea, Costa (kulia) akiwahi mpira baada ya Can kuanguka uwanjani
Costa alionekana akimkita Can katika mguu wa kulia Uwanja wa Stamford Bridge
0 comments:
Post a Comment