MSHAMBULIAJI wa Ivory Coast, Gervinho amefungiwa mechi mbili za Kombe la Mataifa ya Afrika leo, fainali zinazoendelea nchini Equatorial Guine.
Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal, anayecheza Roma kwa sasa, alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja jana baada ya kumzaba kibao kiungo wa Guinea, Naby Keita katika sare ya 1-1 mchezo wa Kundi D.
Lakini kulingana na utaratibu wake, Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limetangaza adhabu hiyo leo, maana yake Gervinho atakosa mechi zote zilizobaki za Kundi D.
Mshambuliaji wa Ivory Coast, Gervinho amefungiwa mechi mbili
0 comments:
Post a Comment