TIMU ya Middlesbrough wamepata zawadi ya ushindi wao wa Kombe la FA Jumamosi dhidi ya mabingwa wa England, Manchester City Uwanja wa Etihad baada yaa kupanhiwa vigogo wengine, Arsenal katika Raundi ya Tatu.
Timu hiyo ya Daraja la Kwanza, ilishinda 2-0 dhidi ya kikosi cha Manuel Pellegrini katika Raundi ya Nne - shukrani kwao wafungaji Patrick Bamford na Kike - na sasa wataifuata The Gunners Uwanja wa Emirates katika hatua ijayo ya mashindano hayo.
Wakati huo huo, mshindi wa mchezo wa marudio wa Raundi ya Nne kati ya Manchester United na Cambridge ya Daraja la Pili, ambazo zilitoka sare Ijumaa atasafiri kuifuata Preston au Sheffield United.
Arsenal itamenyana na Middlesbrough katika Raundi ya Tatu KOmbe la FA
0 comments:
Post a Comment