Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
BINGWA wa michuano ya Kombe la Taifa Wanawake, inayodhaminiwa na kampuni ya Proin na atapata Kombe na fedha taslimu Sh. Milioni 3.
Aidha, katika michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini, mshindi wa pili atapata Sh. Milioni 2, wakati mshindi wa tatu atapata Sh. Milioni 1.
Fainali ya Kombe la Taifa Wanawake itazikutanisha Pwani na Temeke kesho Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam na mashabiki wataingia bure.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mechi hiyo itakayoanza Saa 10.15 jioni, ikichezeshwa na refa wa FIFA, Jonesia Rukyaa na kuonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Azam.
Marefa wasaidizi wanatarajiwa kuwa Hellen Mduma, Agnes Alphonce, na Mwanahamisi Matiku wakati Kamisaa atakuwa Ingridy Kimario.
Timu za Ilala na Kigoma zitacheza mechi ya utangulizi kutafuta mshindi wa tatu kuanzia saa 8.00 mchana.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikuwa mgeni rasmi wakati wa Robo Fainali ya michuano hiyo |
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mechi hiyo itakayoanza Saa 10.15 jioni, ikichezeshwa na refa wa FIFA, Jonesia Rukyaa na kuonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Azam.
Marefa wasaidizi wanatarajiwa kuwa Hellen Mduma, Agnes Alphonce, na Mwanahamisi Matiku wakati Kamisaa atakuwa Ingridy Kimario.
Timu za Ilala na Kigoma zitacheza mechi ya utangulizi kutafuta mshindi wa tatu kuanzia saa 8.00 mchana.
0 comments:
Post a Comment