REAL Madrid imeichapa mabao 4-1 Real Sociedad inayofundishwa na kocha wa zamani wa Manchester United, David Moyes katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Bernabeu leo.
Real Sociedad waliata bao la kushitukiza la kuongoza dakika ya kwanza kupitia kwa Aritz Elustondo, kabla ya James Rodriguez kusawazisha dakika ya tatu.
Sergio Ramos akawafungia wenyeji bao la pili dakikaa ya 36, kabla ya Karim Benzema kufunga la tatu dakika ya 51 na la nne dakika ya 76 kuipa ushindi mnono timu ya Carlo Ancelotti.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo, Irrallamendi, Kroos/Khedira dk81, James/Jese dk74, Isco, Bale na Benzema/Hernandez dk81.
Real Sociedad: Rulli, Aritz/Bergara dk63, Gonzalez, Inigo Martinez, Yuri, Gorka Elustondo, Ruben Pardo, Xabi Prieto, Granero, Canales/De la Bella dk46 na Vela/Agirretxe dk17.
Benzema akikimbia kushangilia baada ya kuifugia Real Madrid bao la tatu dhidi ya Real Sociedad
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2934432/Real-Madrid-4-1-Real-Sociedad-Karim-Benzema-bags-brace-Real-come-goal-inflict-defeat-David-Moyes.html#ixzz3QQZ8XGRf
0 comments:
Post a Comment