BARCELONA imetinga Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme, Hipsania ikijulikana kama Copa del Rey baada ya kuilaza mabao 3-2 Atletico Madrid, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla 4-2.
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Fernando Torres aliifungia Atletico sekunde ya 39, kabla ya Barcelona kusawazisha dakika ya tisa.
Luis Suarez akamsetia Mbrazil, Neymar kuifungia bao la pili Barca, kabla ya Raul Garcia kuisawazishia Atletico Madrid dakika ya 11.
Miranda akajifunga kuipatia bao Barca bao la tatu, kabla ya Gabi kutolewa kwa kadi nyekundu.
Kikosi cha Atletico Madrid; Oblak, Juanfran/Gamez, dk58), Gimenez de Vargas, Miranda, Siqueira; Raul Garcia, Gabi, Suárez, Turan/Cani, dk63), Griezmann/Níguez, dk45 na Torres.
Barcelona; Ter Stegen, Dani Alves, Pique, Mascherano/Mathieu dk61, Alba, Rakitic, Busquets, Iniesta; Messi, Suarez, Neymar/Pedro, 77.
Neymar akishangilia Uwanja wa Vicente Calderon baada ya kuiungia mabao maili katika ushindi wa 3- na Atletico Madrid.
0 comments:
Post a Comment