TIMU ya taifa ya Afrika Kusini imejiweka mguu nje kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika zinazoendelea Eguatorial Guinea baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Senegal usiku huu Uwanja wa Mongomo.
Oupa Manyisa alikaribia kuwa shujaa wa Bafana Bafana baada ya kufunga bao la kuongoxa dakika moja baada ya mapumziko, lakini Kara Mbodji akawasawazishia Simba wa Teranga dakika ya 60.
Sare hiyo inaifanya Bafana Bafana iwe na pointi moja baada ya mechi mbili, kufutaia kufungwa mchezo wa kwanza na Algeria na sasa watalazimika kuifunga Ghana katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi C kuangalia uwezekano wa kuingia 16 Bora.
Mapema katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo Ijumaa, Ghana ilishinda 1-0 dhidi ya Algeria, shukrani kwake mfungaji wa bao hilo, Asamoah Gyan. Senegal inaongoza kundi hilo kwa pointi zake nne, wakati Algeria na Ghana kila moja ina pointi tatu, wakati Bafana inashika mkia kwa pointi yake moja.

0 comments:
Post a Comment