Na Philipo Chimi, SHINYANGA
MABINGWA watetezi, Azam FC wamefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Shukrani kwake, kiungo aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu, Frank Raymond Domayo aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 43 na sasa Azam FC inatimiza pointi 17 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi kwa pointi moja Mtibwa Sugar iliyokuwa juu kwa muda mrefu.
Azam FC ilicheza vizuri na ingeweza kupata mabao zaidi kama washambuliaji wake wangetumia vizuri nafasi walizotengeneza, wakati Stand United licha ya kucheza nyumbani, hawakuwa tishio.
Azam FC sasa inayofundishwa na Mcameroon, Joseph Marious Omog, sasa inaelekea Mwanza, ambako Jumanne itamenyana na Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.
Kikosi cha Stand United kilikuwa; John Mwanda, Revocatus Richard, Yassin Mustafa, Jisend Mathias, Iddi Mobby, Hamisi Shango, Salum Kamana/Tola Mwangonela dk53, Hamisi Thabit/Pastory Athanas dk66, Shaaban Kondo, Heri Mohamed/Chidebele Abasilim dk61 na Mussa Said.
Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Morris, Serge Wawa, Erasto Nyoni/Himid Mao dk77, Mudathir Yahya, Frank Domayo/Kipre Balou dk64, Didier Kavumbangu/Gaudence Mwaikimba dk82, Kipre Tchetche na Brian Majwega.

Frank Domayo (katikati) ameifungia Azam FC bao pekee leo Shinyanga |
Azam FC sasa inayofundishwa na Mcameroon, Joseph Marious Omog, sasa inaelekea Mwanza, ambako Jumanne itamenyana na Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.
Kikosi cha Stand United kilikuwa; John Mwanda, Revocatus Richard, Yassin Mustafa, Jisend Mathias, Iddi Mobby, Hamisi Shango, Salum Kamana/Tola Mwangonela dk53, Hamisi Thabit/Pastory Athanas dk66, Shaaban Kondo, Heri Mohamed/Chidebele Abasilim dk61 na Mussa Said.
Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Morris, Serge Wawa, Erasto Nyoni/Himid Mao dk77, Mudathir Yahya, Frank Domayo/Kipre Balou dk64, Didier Kavumbangu/Gaudence Mwaikimba dk82, Kipre Tchetche na Brian Majwega.
0 comments:
Post a Comment