// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC NA MTIBWA SUGAR ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC NA MTIBWA SUGAR ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, January 06, 2015

    AZAM FC NA MTIBWA SUGAR ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

    Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
    AZAM FC itakutana na Mtibwa Sugar katika Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi keshokutwa kufuatia kumaliza nafasi ya pili katika Kundi B, nyuma ya mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda.
    Azam FC imeshinda 1-0 katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi B dhidi ya Mtende Rangers uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar jioni ya leo.
    Hadi mapumziko, Azam FC walikuwa tayari wamekwishapata bao hilo lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu dakika ya 34 akimalizia krosi ya winga wa kimataifa wa Uganda, Brian Majwega.
    Didier Kavumbangu kulia akipongezwa na Frank Domayo na John Bocco baada ya kuifungia Azam FC leo

    Kavumbangu alifunga bao hilo kiasi cha dakika nane tangu aingie uwanjani kwenda kuchukua nafasi ya Kelvin Friday ambaye mchezo ulimkataa leo na kocha Joseph Marius Omog akaamua kumpumzisha mapema.
    Katika mechi zilizotangulia, mabingwa watetezi, KCCA ya Uganda waliwafunga KMKM 2-1 mchezo wa Kundi B, wakati Polisi iligawana pointi na Taifa Jang’ombe kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Mao dze Tung.
    Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Aggrey Morris, Serge Wawa, Mudathir Yahya/Shomary Kapombe dk, Frank Domayo, Brian Majwega, Himid Mao/Farid Mussa dk70, John Bocco/Amri Kiemba dk78na Kelvin Friday/Didier Kavumbangu dk26.
    Mtende Rangers; Juma Machano, Suleiman Juma, Amour Hajji, Ali Mohammed, Mussa Said, Suleiman Said, Twaha Rajab, Ujata Makoba/Herman Kunambi dk59, Jumanne Seif, Saleh Ahmed/Abeid Salum dk66 na Mussa Digubike.
    Didier Kavumbangu akimtoka beki wa Mtende Rangers
    Frank Domayo katikati ya wachezaji wa Mtende

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC NA MTIBWA SUGAR ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top