KALBU ya Arsenal imemsajili kiungo kinda, Krystian Bielik kutoka Legia Warsaw.
Timu hiyo ya Ligi Kuu ya England imethibitisha usajili wa kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 kupitia tovuti yake rasmi, ikisema imetumia Paunu Milioni 2.5.
Mwanasoka kijana wa kimataifa wa Poland, Bielik, ambaye aliwahi pia kufanya mazungumzo na Hamburg ya Ujerumani, anatarajiwa kuchezea kwa muda timu ya vijana ya Arsenal chini ya umri wa miaka 21, kabla ya kupandishwa kikosi cha wakubwa.
Krystian Bielik akiwa amepozi na jezi ya Arsenal baada ya kukamilisha usajili wake kutoka Legia Warsaw
0 comments:
Post a Comment