KLABU ya Arsenal imekataa ofa ya kumsajili kiungo wa Newcastle, kiungo Cheick Tiote.
The Gunners wamepewa ofa ya kumsajili kiungo huyo wa Ivory Coast kuelekea kufungwa dirisha dogo la usajili Jumatatu.
Lakini wamekataa ifa hiyo ya kumsajili kiungo huyo mkabaji na japokuwa kocha Arsene Wenger anataka kiungo wa aina ya Tiote, lakini amesema anataka mkali kuliko huyo.
Tiote, ambaye anaweza kugharimu Pauni Milioni 12, yuko huru kuondoka St James' Park akapate changamoto mpya.
Arsenal imemkataa kiungo wa Newcastle, Cheick Tiote
0 comments:
Post a Comment