ARSENAL wamewakalisha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester City kwa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Etihad usiku huu.
Ushindi huo, unaifanya The Gunners ifikishe pointi 39 baada ya mechi 22 na kupanda hadi nafasi ya tano mbele ya Tottenham, wakati City inayobaki na pointi zake 47 inaendelea kukamata nafasi ya pili.
Santi Carzolla alifungua biashara kwa bao la penalti dakika ya 24, kufuatia Nahodha wa City, Vincent Kompany kumchezea rafu Nacho Monreal kwenye eneo la hatari.
Olivier Giroud akakamilisha ushindi wa pointi tatu muhimu kwa kikosi cha Arsene Wenger kwa bao la pili dakika ya 66.
Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Fernandinho/Lampard dk63, Fernando, Jesus Navas/Dzeko dk76, Silva, Milner/Jovetic dk46 na Aguero.
Arsenal: Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Oxlade-Chamberlain/Rosicky dk66, Ramsey/Flamini dk84, Cazorla, Sanchez/Gibbs dk84 na Giroud.
Giroud akiteleza kushangilia na mchezaji mwenzake wa Arsenal, Alexis Sanchez baada ya kufunga
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2915617/Manchester-City-0-2-Arsenal-Santi-Cazorla-s-penalty-Olivier-Giroud-s-header-earn-Gunners-rare-victory-Etihad-Stadium.html#ixzz3PCLPnFyC
0 comments:
Post a Comment