WINGA wa kimataifa wa Uholanzi, Arjen Robben amefunga mabao mawili jana katika ushindi wa 5-1 wa Bayern Munich akisherehekea kutimiza miaka 31 ya kuzaliwa.
Bayern inayofundishwa na kocha Mspanyola, Pep Guardiola imecheza mechi moja tu tangu katikati ya Desemba - ya kirafiki nchini Saudi Arabia - kabla ya jana kuifumua timu ya Daraja la Pili Bochum, kuelekea mzunguko wa pili wa Bundesliga ambao wataanza na Wolfsburg wikiendi ijayo.
Danny Latza alianza kuifungia Bochum, kabla ya Arjen Robben kuisawazishia Bayern, Dante akafunga la pili, Mario Gotze la tatu, Robben tena la nne na Sebastian Rode akakamilisha la tano.
Arjen Robben akitabasamu wakati wa mechi mjini Bochum jana kufuatia kufunga mabao mawili akitimiza miaka 31 ya kuzaliwa
0 comments:
Post a Comment