KOCHA wa zamani wa West Ham na Watford, Gianfranco Zola ameteuliwa kuwa kocha wa klabu ya Serie A, Cagliari.
Zola, mwenye umri wa miaka 48, awali aliichezea klabu hiyo kwa misimu yake miwili ya mwisho kama mchezaji baada ya kuichezea Chelsea kwa miaka saba.
Mapema wiki hii, La Gazzetta dello Sport liliandika kwamba gwiji huyo mwenye umri wa miaka 48 alikuwa mbioni kujiunga na timu hiyo ya Serie A na sasa yametimia.
Kocha wa zamani wa Watford na West Ham, Gianfranco Zola
0 comments:
Post a Comment