MWANASOKA bora wa zamani wa Dunia, Zinadine Zidane amekutana na mashujaa wenzake walioipa Ufaransa Kombe la mwaka 1998 na kupiga nao picha ya pamoja ya kumbukumbu wakiwa wameizunguka meza kwa chakula cha usiku.
Zinedine Zidane ameposti picha hiyo na kikosi cha ubingwa wa Kombe la dunia mwaka mjini Paris jana usiku, akiwa na nyota wenzake wa enzi hizo kama Laurent Blanc, Fabien Barthez, Didier Deschamps na Lilian Thuram.
"Ufaransa 98 mjini Paris! Chakula cha usiku na marafiki wakubwa na wachezaji ndani ya Paris!" ameandika Zidane kama maelezo ya picha hiyo katika akaunti yake ya Instagram.
Zinedine Zidane ameposti hii picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa na wachezaji wenzake walioipa Ufaransa Kombe la Dunia mwaka 1998 mjini Paris. (Mbele, kutoka kushoto) Laurent Blanc, Bixente Lizarazu, Zidane, Christian Karembeu, Bernard Diomede, Ludovic Giuly. Nyuma kutoka kulia) Lilian Thuram, Bernard Lama, Frank Leboeuf, Didier Deschamps, Christophe Dugarry, Sabri Lamouchi na Fabien Barthez.
Kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 1998 kwa kuifunga Brazil fainali mabao 3-0. (Juu kutoka kushoto: Zinedine Zidane, Marcel Desailly, Frank Leboeuf, Lilian Thuram, Stephane Guivarc'h, Emmanuel Petit; waliochuchumaa kutoka kushoto ni Christian Karembeu, Youri Djorkaeff, Didier Deschamps, Fabien Barthez na Bixente Lizarazu)
Zidane alikuwa nyota wa timu hiyo iliyotamba katika fainali zilizofanyika nyumbani wakiifunga Brazil 3-0 mechi ya mwisho na kutwaa taji lao la kwanza na pekee la Kombe la Dunia.
Zizou, aliyefunga mabao mawili kwenye fainali pichani ameketi na mabeki Bixente Lizarazu na Blanc, ambaye kwa sasa ni kocha wa Paris Saint-Germain.
Katika bega lake lingine kuna kiungo Christian Karembeu, anayefanya kazi Olympiacos ya Ugiriki, Bernard Diomede na Ludovic Giuly, ambaye hakuwemo kwenye kikosi cha 1998.
Nyuma yao kuna beki Thuram, kipa wa pili Bernard Lama, Leboeuf, Deschamps, Christophe Dugarry, Sabri Lamouchi, ambaye hakuwemo kwenye kikosi cha mwisho na Barthez.
0 comments:
Post a Comment