MWANASOKA wa kimataifa wa Algeria, Yacine Brahimi (pichani juu na tuzo yake) amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC) kwa Afrika mwaka 2014.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 anakuwa Mualgeria wa kwanza kushinda tuzo hiyo ambayo inatokana na kura za mashabiki.
Winga huyo wa Porto ya Ureno amesema baada ya kushinda tuzo hiyo; "Ni heshima kubwa kwangu kupokea tuzo hii, hii ni tuzo babu kubwa. Naikabidhi kwa nchi yangu, Algeria, na watu wote walionipigia kura mimi.
"Pia ni taji kwa ajili ya Waafrika wote, kwa sababu ni kwa ajili ya mchezaji wa Afrika. Hivyo, nina furaha sana,” amesema.
Baada ya kupata kura kibao za rekodi kutoka nchi 207 wanachama wa FIFA, Brahimi amefanikiwa kuwapiku Mnigeria Vincent Enyeama, Mgabon Pierre-Emerick Aubameyang na Gervinho na Yaya Toure wote wa Ivory Coast.
Brahimi alikuwa ana mchango kwa mafanikio ya klabu na timu yake ya taifa, Algeria kwanza kufuzu Kombe la Dunia na pili kufika hatua ya 16 Bora kwa mara ya kwanza. Kombe la Dunia ndipo alipofunga bao lake la kwanza katika timu yake ya taifa ikishinda 4-2 dhidi ya Korea Kusini hatua ya makundi.
WASHINDI WA AWALI TUZO YA MWANASOKA BORA WA BBC AFRIKA
2013: Yaya Toure (Manchester City & Ivory Coast)
2012: Chris Katongo (Henan Construction & Zambia)
2011: Andre Ayew (Marseille & Ghana)
2010: Asamoah Gyan (Sunderland & Ghana)
2009: Didier Drogba (Chelsea & Ivory Coast)
2008: Mohamed Aboutrika (Al Ahly & Misri)
2007: Emmanuel Adebayor (Arsenal & Togo)
2006: Michael Essien (Chelsea & Ghana)
2005: Mohamed Barakat (Al Ahly & Misri)
2004: Jay-Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
2003: Jay-Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
2002: El Hadji Diouf (Liverpool & Senegal)
2001: Sammy Kuffour (Bayern Munich & Ghana)
2000: Patrick Mboma (Parma & Cameroon)

Yacine Brahimi aliisaidia Algeria kufuzu Kombe la Dunia na baadaye kufika 16 Bora kwa mara ya kwanza |
WASHINDI WA AWALI TUZO YA MWANASOKA BORA WA BBC AFRIKA
2013: Yaya Toure (Manchester City & Ivory Coast)
2012: Chris Katongo (Henan Construction & Zambia)
2011: Andre Ayew (Marseille & Ghana)
2010: Asamoah Gyan (Sunderland & Ghana)
2009: Didier Drogba (Chelsea & Ivory Coast)
2008: Mohamed Aboutrika (Al Ahly & Misri)
2007: Emmanuel Adebayor (Arsenal & Togo)
2006: Michael Essien (Chelsea & Ghana)
2005: Mohamed Barakat (Al Ahly & Misri)
2004: Jay-Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
2003: Jay-Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
2002: El Hadji Diouf (Liverpool & Senegal)
2001: Sammy Kuffour (Bayern Munich & Ghana)
2000: Patrick Mboma (Parma & Cameroon)
0 comments:
Post a Comment