Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
VIINGILIO vya pambano la Nani Mtani Jembe 2 kati ya Simba na Yanga linalodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager litakalochezwa Jumamosi, Desemba 13, 2014 kuanzia Saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, vimetajwa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Meneja Udhamini wa TBL, George Kavishe amesema kwamba kiingilio cha chini kitakuwa Sh. 7,000.
“Tayari Simba na Yanga zimesaini makubaliano ya kucheza mechi ya Nani Mtani Jembe 2 (Nani Mtani Jembe 2 Match). Pambano hili nihitimisho la kampeni ya NMJ iliyoendeshwa kwa wiki 10 ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kila wanapoburudika na bia ya Kilimanjaro Premium Lager na vilevile ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia sahihi makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
Meneja Masoko wa Yanga SC, George Simba katikati akizungumzia mechi hiyo. Kushoto ni Ofisa Habari wa Simba SC |
• Kampeni hii inaendeshwa kwa njia ya sms ambapo mashabiki wanapiga kura kwa njia ya sms na ambapo shilingi milioni 80 zimegawanywa kati ya timu hizo mbili kwa kiasi cha sh milioni 40 kwenye benki maalumu mtandaoni.
• Shilingi Milioni 20 ni zawadi ya mechi ya Nani Mtani Jembe ambapo timu itakayoshinda itapata sh milioni 15 na timu itakayofungwa itapata shilingi milioni 5.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli alisema mashabiki wa Simba na Yanga wanaweza kushiriki kwa kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager yenye ujazo wa mililita 500 ambapo mteja atabandua ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager na kuona namba maalumu. Ataandika jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo ya kwenye kizibo ambayo anatuma kwenda namba 15415 na kwa kufanya hivyo anakuwa amepunguza pesa taslimu shilingi 10,000/= kutoka timu pinzani na kuichangia timu yake.
Kikuli pia aliwahimiza mashabiki waendelee kuzipigia kura timu zao na kikubwa kuhakikisha wanafika uwanja wa taifa na kujionea wenyewe pambano hilo ambalo lazima mshindi apatikane.
Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura aliwakaribisha mashabiki na kuwaomba wajitokeze kwa wingi kwani hivi sasa timu hizo ziko kambini zikijiandaa na mtanage huo wa kukata na shoka unaotarajiwa kuwa na msisimko mkubwa.
Wambura alitaja viingilio vya mechi hiyo kuwa ni shilingi 30,000 kwa VIP B, 20,000/= VIP C, 15,000/= kwa viti vya rangi ya chungwa kiingilio kitakuwa ni sh 15,000 huku viti vya bluu na kijani tiketi zikiuzwa kwa sh. 7,000/=.
Wambura alisema pambano hilo litakalosimamiwa na TFF litaanza saa kumi kamili na litachezwa kwa dakika 90 tu ambapo kama muda timu hizo hazitafungana basi mikwaju ya penati itapigwa ili mshindi apatikane.
Taji la Nani Mtani Jembe linashikiliwa na Simba ambao waliwafunga mahasimu wao 3-1 katika mechi iliyochezwa Disemba 21, 2013.
Meneja wa Bia ya Kilimajaro, Pamela Kikuli (katikati) akizungumzia mechi hiyo. Kushoto ni Mkurgenzi wa Mashindano wa TFF, Boniphace Wambura na kulia Meneja Udhamini wa TBL, George Kavishe |
0 comments:
Post a Comment