MSHAMBULIAJI Fernando Torres anatarajiwa kujiunga na klabu yake iliyomuibua kisoka, Atletico Madrid baada ya kufikia makubaliano na AC Milan ambao watamchukua Alessio Cerci kutoka timu hiyo.
Milan imethibitisha katika Televisheni yake kwamba mazungumzo yamefanyika na makubaliano yamefikiwa, hivyo kinachosubiriwa ni utekelezaji wake.
Torres yuko katika Mkataba wa mkopo wa miaka miwili kutoka Chelsea, lakini ameshindwa kuvutia Milan na Atletico wanashawishika kwamba El Nino anaweza kufufua makali yake akirejea kucheza Hispania. Waatauchukua wao Mkataba wa mkopo wa Chelsea na kumsaini kwa miezi 18 Torres.
Fernando Torres atajiunga na klabu yake ya zamani, Atletico Madrid baada ya kushindwa kuonyesha cheche AC Milan
Torres yuko katika Mkataba wa mkopo wa miaka miwili kutoka Chelsea
Cerci, aliyejiunga na Atletico kwa dau la Pauni Milioni 13 msimu huu kutoka Torino, atakwenda Milan inayomchukua badala ya Torres.
Torres aliibukia Atletico mwaka 2001 ambako baada ya kufunga mabao 82 katika mechi 214 alizocheza, mwaka 2007 akahamia Liverpool alikocheza mechi 102 na kufunga mabao 65.
Torres alikuwa mwenye mafanikio Liverpool na haikuwa ajabu alipouzwa kwa dau la rekodi Uingereza Pauni Milioni 50 kwenda Chelsea, ambako ndiko cheche zake zilipopotelea.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania, alifunga mabao 20 katika mechi 110 alizocheza Stamford Bridge, kabla hya kutolewa kwa mkopo msimu huu kwenda Milan, ambako baada ya mechi 10 amefanikiwa kufunga bao moja tu.
0 comments:
Post a Comment