MSHAMBULIAJI Fernando Torres jana amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza tangu arejee Atletico Madrid.
Mpachika mabao huyo amnaye nyota yake imefifia kwa sasa, amekamilisha uhamisho wa mkopo kutoka AC Milan mapema wiki hii na anatarajiwa kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Levante Jumamosi.
Awali, Mspanyola huyo alipata mapokezi mazuri wakati anawasili Uwanja wa Ndege wa Barajas mjini Madrid.
Fernando Torres akifanya mazoezi na Atletico Madrid mjini Majadahonda, jirani na Madrid kwa mara ya kwanza tangu arejee
Torres akijibu maswali ya Waandishi wa Habari baada ya kuwasili Madrid
Jumatatu, Torres alitweet juu ya namna alivyovutiwa kurejea katika klabu iliyomuibua akiwa kinda.
Kwenye akaunti yao ya Instagram, Atletico Madrid wametangaza furaha yao juu ya kurejea kwa mshambuliaji huyo.
Mabingwa hao wa La Liga wameandika: 'Fernando @Torres ametua Uwanja wa Ndege wa Barajas. Anawasalimia wote.'
Torres, mwenye umri wa miaka 30, amekubali kujiunga tena na klabu yake ya utotoni kwa mkopo kutoka AC Milan Jumatatu na atakuwa huko hadi mwisho wa msimu wa 2015-2016.
Alipokuwa katika klabu hiyo mara ya kwanza, mshindi huyo wa Kombe la Dunia alicheza mechi 214 Atletico na kufunga mabao 84. Mechi yake ya kwanza baada ya kurejea inatarajiwa kuwa dhidi ya wapinzani wao wa Jiji, Real kwenye 16 Bora ya Kombe la Mfalme Januari 7, mwakani ingawa mabingwa hao wa La Liga wanatarajiwa kucheza na Levante Januari 3.
0 comments:
Post a Comment