MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Daniel Sturridge ametumia akaunti yake ya Instagram kuthibitisha namna anavyojifua ili kuwa fiti tena.
Mpachika mabao huyo wa Liverpool anafanya mazoezi mjini Los Angeles, Marrkani ili kupona maumivu yake ya mguu aweze kurejea uwanjani akiwa fiti zaidi.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 25 amepelekwa Marekani ili kwenda kuendelea kupambana na maumivu yake ambayo yamemuweka nje kwa muda mrefu msimu huu. Sturridge ameposti picha zake akiwa anajifua kwenye gym.
Daniel Sturridge ameposti picha Instagram kuwaambia mashabiki kwamba atarejea akiwa fiti zaidi
Picha tofauti ambazo nyota huyo wa Liverpool ameposti akiwa gym anajifua
0 comments:
Post a Comment