Na Mwandishi Wetu, ACCRA
NAHODHA wa zamani wa Ghana, Stephen Appiah ameionya timu yake hiyo ya taifa, Black Stars kwamba ikifanya mzaha katika maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika 2015, haitafika popote.
Baada ya droo iliyopangwa Jumatano iliyopita, timu hiyo kutoka Magharibi mwa Afrika imepangwa pamoja na Afrika Kusini, Algeria na Senegal.
“Tuache kujidanganya wenyewe, hili ni kundi gumu mno, Tunaweza kutoka? Ndiyo. Tunatakiwa kujiandaa kwa ajili hiyo kuanzia mchezo wa kwanza dhidi ya Senegal,”amesema.
Ametaka maandalizi ya mazuri yafanyike na mikakati thabiti iwekwe ili kikosi cha Ghana kiweze kusonga mbele kutoka kwenye kundi hilo linaloitwa la kifo.
“Tuna fainali tatu tatu katika harua ya makundi. Ghana ina uwezo wa kufunga nchi yoyote duniani katika siku yetu, lakini wote tunatakiwa kufanya kazi makini sasa,” amesema.
“Muda si rafiki kwetu, lakini acha tujiandae kikamilifu na tutafuzu,” amesema akizungumza na mtandao wa Ghanasoccernet. Michuano hiyo itafanyika nchini Equatorial Guinea kuanzia Januari 17, mwakani.

Stephen Appiah ameiasa Ghana ifanye maandalizi mazuri kuelekea AFCON |
Ametaka maandalizi ya mazuri yafanyike na mikakati thabiti iwekwe ili kikosi cha Ghana kiweze kusonga mbele kutoka kwenye kundi hilo linaloitwa la kifo.
“Tuna fainali tatu tatu katika harua ya makundi. Ghana ina uwezo wa kufunga nchi yoyote duniani katika siku yetu, lakini wote tunatakiwa kufanya kazi makini sasa,” amesema.
“Muda si rafiki kwetu, lakini acha tujiandae kikamilifu na tutafuzu,” amesema akizungumza na mtandao wa Ghanasoccernet. Michuano hiyo itafanyika nchini Equatorial Guinea kuanzia Januari 17, mwakani.
0 comments:
Post a Comment