BAO pekee la Alexis Sanchez kwa mara nyingine limethibitisha thamani yake Arsenal baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Southampton Uwanja wa Emirates.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Chile, alifunga bao hilo pekee dakika ya 89 akimalizia kazi nzuri ya Aaron Ramsey baada ya wageni kubaki 10 kufuatia kuumia kwa Toby Alderweireld wakati wamemaliza idadi ya wachezaji wa kubadili.
Ushindi huo wa kikosi cha Arsene Wenger unaipeleka timu hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, wakati Southampton inabaki nafasi ya tatu, mbele ya Manchester United.
Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez (mbele) akimtoka beki wa Southampton, Nathaniel Clyne
Mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck (katikati) akipambana kwenye eneo la hatari la Southampton
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2859811/Arsenal-1-0-Southampton-Alexis-Sanchez-proves-Gunners-hero-late-winner-moves-sixth.html#ixzz3KsIEkKeX
Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook
0 comments:
Post a Comment