NAHODHA Wayne Rooney leo atakwenda kufanyiwa vipimo wakati wachezaji wenzake wengine wote wa Manchester United wanajiandaa kuingia kwenye sherehe za Krisimasi.
Rooney aliukosa mchezo wa jana usiku United ikishinda 2-1 dhidi ya Stoke City baada ya kuumia mwishoni mwa mchezo dhidi ya Hull, na kocha Louis van Gaal sasa anasubiri kujua kama Nahodha wake atakuwepo kwenye mechi ya Jumatatu dhidi ya Southampton.
"Tunatakiwa kusubiri hadi Jumatano ili kuweza kusema chochote juu yake (Rooney) kwa sababu huwezi kujua juu ya goti lake,"amesema Van Gaal.
Wayne Rooney akiiangalia Manchester United ikiifunga Stoke jana yeye akiwa jukwaani baada ya kuumia goti dhidi ya Hull
0 comments:
Post a Comment