WINGA wa Bayern Munich ya Ujerumani, Arjen Robben amekuwa Mwanamichezo Bora wa Mwaka wa Uholanzi, wakati kocha wa Manchester United Louis van Gaal amekuwa kocha bora wa nchi hiyo.
Katika shetehe za tuzo jana mjini Amsterdam, mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie ameshinda kutokana na bao lake bora la kichwa dhidi ya Hispania katika Kombe la Dunia.
Van Vaal amapata tuzo hiyo baada ya kuiongoza hadi Nusu Fainali Uholanzi kwenye Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil. Dereva kinda wa miaka 17, Max Verstappen ameshinda tuzo ya Mwanamichezo Chipukizi, wakati Ireen Wust ndiye Mwanamichezo Bora wa Kike Uholanzi mwaka 2014 baada ya kufanya vizuri kwenye Olimpiki.
Robin van Persie (katikati) akipokea tuzo yake kutoka Danny Blind na kushoto ni kocha Louis Van Gaal
Winga wa Bayern Munich alitokea kwenye TV kubwa kupokea tuzo yake jana usiku
0 comments:
Post a Comment