MWANASOKA bora wa kike wa dunia mara tano, Marta amepata ajali ya gari nchini Brazil.
Nyota huyo wa timu ya taifa ya wanawake wa Brazil alipelekwa hospitali kwa vipimo, lakini ikagundulika hajapata madhara makubwa na akaruhusiwa baada tu ya ajali hiyo Jumamosi.
Tukio hilo lilitokea Kaskazini Mashariki mwa Brazil, ambako nyota huyo alikwenda kwa ajili ya mapumziko. Mamlaka zimesema kwamba Marta alipoteza mwelekeo wakati anaendesha gari lake aina ya Audi na kulipeleka pembezoni mwa barabara.
Nyota wa Brazili, Marta amepata ajali akiwa mapumzikoni
Tovuti ya GloboEsporte imeandika kwamba watu wengine watatu waliokuwamo kwenye gari hilo hawakuumia sana pia.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 ameripotiwa kwamba alikuwa anarejea kutoka nyumbani kwa rafiki yake wakati ajali hiyo inatokea mchana katika mji wa Santana do Ipanema.
Marta ataichezea Brazil katika mashindano ya kimataifa mji Mkuu wa nchi hiyo, Brasilia wiki hii.
Mwanasoka Bora wa Dunia mara tano anatarajiwa kuichezea timu ya taifa ya wanawake ya Brazil wiki hii
0 comments:
Post a Comment