Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KIUNGO wa Azam FC anayemudu kucheza na nafasi za ulinzi pia, ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), wakati Sheridah Boniface amekuwa Mwanamichezo bora wa Mwaka 2014.
Nyoni aliyeibukia Vital’O ya Burundi, ameshinda tuzo baada ya kuwangusha Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ na mshambuliaji wa Simba SC, Elias Maguli.
Katika hafla iliyofanyika usiku huu ukumbi wa VIP Diamond Jubilee, Dar es Salaam Mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alimkabidhi tuzo maalum, mke wa Rais wa kwanza wa visiwa hivyo, mama Fatuma Karume kwa ajili mumewe, marehemu Abeid Amaan Karume.
Mzee Karume ameshinda tuzo maalum ya watu waliotoa mchango mkubwa kwenye michezo- ikiwa ni pamoja na kuziwezesha Simba SC na Yanga kuwa majengo yao.
Mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta ameshinda tuzo ya Mwanamichezo Bora anayecheza nje, wakati Kipre Herman Tchetche wa Ivory Coast, amewashinda Mbuyu Twite Rwanda na Amisi Tambwe wa Burundi katika tuzo ya Mwanasoka wa kigeni nchini.
Sheridah Boniface ameshinda tuzo tatu, Mwanamichezo Bora wa Jumla, Mwanasoka Bora wa kike na mwanamichezo Bora Chipukizi, Novatus Emanuel ameshinda katika Tenisi ya Walemavu wanaume na kwa wanawake Rehema Said, Magongo wameshinda Joan Wilson na Kidawa Suleiman, Wavu wameshinda Teddy Mgwao na Kevin Peter, Riadha ni Alphonce Felix na Zakia Mrisho.
Katika kikapu ni Kikapu ahmed, wakati katika netiboli ni Dolita Mbunda, Kuogelea mshindi ni Hilal Hilal na Catherine Mason, mshindi wa judo, Godfrey Mtao na Grace Mhanga.
Katika tenisi, Omar Sule na Rehema Athumani, ngumi za kulipwa ni Francis Cheka, ridhaa Suleiman Kidunda.
Mshindi wa gofu ya kulipwa Hassan Kadio wakati kwa ridhaa Nuru Mollel, baiskeli Sofia...na Richard Laizer; mikono ni Ahmed Saleh na Veronica Mapunda, Olimpiki maalumu ni Raphael Kalukula na Brandina Brasi.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) kulia akimkabidhi Erasto Nyoni tuzo ya Mwanasoka Bora |
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein akimkabidhi Mama Fatuma Karume Tuzo ya Heshima, kwa ajili ya marehemu mumewe, Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amaan Karume |
Mzee Karume ameshinda tuzo maalum ya watu waliotoa mchango mkubwa kwenye michezo- ikiwa ni pamoja na kuziwezesha Simba SC na Yanga kuwa majengo yao.
Mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta ameshinda tuzo ya Mwanamichezo Bora anayecheza nje, wakati Kipre Herman Tchetche wa Ivory Coast, amewashinda Mbuyu Twite Rwanda na Amisi Tambwe wa Burundi katika tuzo ya Mwanasoka wa kigeni nchini.
Sheridah Boniface ameshinda tuzo tatu, Mwanamichezo Bora wa Jumla, Mwanasoka Bora wa kike na mwanamichezo Bora Chipukizi, Novatus Emanuel ameshinda katika Tenisi ya Walemavu wanaume na kwa wanawake Rehema Said, Magongo wameshinda Joan Wilson na Kidawa Suleiman, Wavu wameshinda Teddy Mgwao na Kevin Peter, Riadha ni Alphonce Felix na Zakia Mrisho.
Katika kikapu ni Kikapu ahmed, wakati katika netiboli ni Dolita Mbunda, Kuogelea mshindi ni Hilal Hilal na Catherine Mason, mshindi wa judo, Godfrey Mtao na Grace Mhanga.
Katika tenisi, Omar Sule na Rehema Athumani, ngumi za kulipwa ni Francis Cheka, ridhaa Suleiman Kidunda.
Mshindi wa gofu ya kulipwa Hassan Kadio wakati kwa ridhaa Nuru Mollel, baiskeli Sofia...na Richard Laizer; mikono ni Ahmed Saleh na Veronica Mapunda, Olimpiki maalumu ni Raphael Kalukula na Brandina Brasi.
0 comments:
Post a Comment