CHELSEA imeendelea vyema na mawindo yake ya taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tottenham Hotspur usiku huu Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Eden Hazard aliifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 19, akimtungua Hugo Lloris ndania ya boksi, kabla ya mkongwe Didier Drogba kufunga la pili dakika tatu baadaye.
Gary Cahill alilazimika kutoka nje mapumziko baada ya kuumia kichwani kufuatia kugongana na Jan Vertonghen na Loic Remy akatokea benchi kuchukua nafasi ya Drogba na kuifungia Chgelsea bao la tatu 73.
Matoeko haya ni muendelezo wa unyonge wa Tottenham kwenye himaya Chelsea, kwani Spurs hawajashinda Uwanja wa Stamford Bridge kwenye Ligi Kuu ya England kwa miaka 24 sasa.
Didier Drogba akimtoka Jan Vertonghen kabla ya kuifungia Chelsea katika ushindi wa 3-0 usiku huu
Drogba akishangilia kwa staili yake maarufu Stamford Bridge
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2859615/Chelsea-3-0-Tottenham-Eden-Hazard-Didier-Drogba-Loic-Remy-lead-Blues-cruise.html#ixzz3KsMOKbvn
0 comments:
Post a Comment