BINGWA wa zamani wa ngumi za uzito wa juu mara tatu duniani, Muhammad Ali amepelekwa hospitali kwa maradhi ya Nimonia, ingawa inaelezwa hali yake si mbaya.
Ali, ambaye anapambana na maradhi ya Kiharusi, amekuwa akitibiwa na timu ya madaktari wake na yupo katika hali nzuri, amesema Msemaji wake, Bob Gunnell.
"Alikwenda hospitali asubuhi ya leo (Jumamosi),"amesema Gunnell.
"Kwa sababu Nimonia iligundulika mapema, maendeleo yake ni mazuri na anatarajiwa kuwa hospitali kwa muda mfupi,".
Ali alitokea hadharani Septemba kuhudhuria sherehe katika mji wake, Louisville za tuzo za Muhammad Ali Humanitarian, lakini hakuzungumza. Ali alistaafu ngumi mwaka 1981 na kujiingiza kwa shughuli za kijamii.
0 comments:
Post a Comment