KOCHA Jose Mourinho amewalalamikia waokota mipira wa Newcastle kuchelewesha mipira baada ya timu yake, Chelsea kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa St James' Park jana.
Mourinho, ambaye hajawahi kuonja ushindi mbele ya Newcastle katika awamu zake mbili za kufanya kazi Chelsea, amesema timu yake haikuwa na bahati hadi kupoteza mchezo huo jana dhidi ya The Magpies, akilalamikia zaidi mbinu za kuchelewesha muda za wapinzani wao.
Papiss Cisse alitokea benchi kuifungia mabao yote Newcastle, wakati bao pekee la The Blues lilifungwa na mkongwe Didier Drogba.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akizungumza na refa wa akiba, Robert Madley jana
"Hakuna malalamiko. Hatukuwa na bahati,"amesema. "Tulipata nafasi nyingi za kufunga kipindi cha kwanza, hatukufunga. Kipindi cha pili, tena tulipata nafasi, hatukuweza (kufunga).
"Walipaki basi, na mara ya kwanza walikuwa kule (kwenye kushambulia) wakapata bao. Baada ya hapo, kila mtu akawa nyuma ya mpira dhidi ya timu ambayo ilipambana hadi dakika ya mwisho kwa kila mchezaji kujitolea kusaka mabao,"amesema Mourinho.
Kipigo cha jana kinaounguza idadi ya pointi ambazo vinara hao wa Ligi Kuu ya England wanawazidi mabingwa watetezi, Manchester City hadi kubaki tatu- na maana yake mbio za ubingwa sasa zimekolea uhondo.
0 comments:
Post a Comment