LIVERPOOL imewafumua mabao 3-1 wenyeji Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa King Power usiku huu.
Nahodha Steven Gerrard leo alianzishwa kwenye kikosi cha kwanza baada ya kutupwa benchi mwishoni mwa wiki dhidi ya Stoke- na shuti la
Leonardo Ulloa liligonga mwamba kabla ya Simon Mignolet kujifunga katika harakati za kuokoa kuipatia Leicester bao la kwanza dakika ya 22.
Adam Lallana akaisawazishia Liverpool dakika nne baadaye baada ya ushrikiano mzuri na mchezaji mwenzake wa zamani wa Southampton, Rickie Lambert
Mkongwe, Gerrard akawafungia Wekundu hao bao la pili dakika ya 54, kabla ya Jordan Henderson kufunga la tatu dakika ya 83 kwa Liverpool.
Kikosi cha Leicester kilikuwa: Schmeichel, De Laet, Morgan, Wasilewski, Konchesky/Albrighton, Schlupp, Cambiasso, James, Mahrez, Vardy na Ulloa.
Liverpool; Mignolet, Manquillo/Moreno, Skrtel, Toure, Johnson, Lucas, Henderson, Sterling/Lovren, Gerrard, Lallana/Allen na Lambert.
Steven Gerrard (kulia) akishangilia baada ya kuifungia Liverpool katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Leicester
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2858105/Leicester-1-3-Liverpool-Steven-Gerrard-Captain-scores-return-Adam-Lallana-Jordan-Henderson-aid-Reds-revival.html#ixzz3KmUHN4Yh
0 comments:
Post a Comment