Unakumbuka kile kipindi maarafu cha Radio Tanzania (RTD) cha Pwangu na Pwaguzi? Unakumbuka namna wahusika wa kipindi hicho walivyokuwa na mipango mingi ambayo mwisho wa siku ilikuwa haizai matunda? Ndivyo wakati mwingine ninavyofananisha baadhi ya bendi za dansi na taarab na kipindi hicho cha Pwagu na Pwaguzi.
Kuna tofauti moja kubwa sana kati ya muziki wa taarab na wa dansi kibiashara, ambayo pengine watu wengi hawaifahamu.
Makundi ya dansi na taarab yanafanana linapokuja suala la kutumbuiza kwenye kumbi, lakini yanatofautina sana nje ya hapo, namaanisha kukubalika kwa muziki wao uraiani – majumbani, kwenye sherehe pamoja na kwenye vyombo vya habari kama vile radio na televisheni. Taarab inakubalika sana kwenye jamii, inakubalika sana kwenye vyombo vya habari, lakini kwa bahati mbaya mashabiki wao wengi ni wale wanaopenda kuburudika wakiwa majumbani badala ya kuhudhuria kwenye kumbi za starehe.
Kwenye kumbi ni bendi mbili au tatu za taarab ndio zinafanya vizuri, lakini zilizobakia hali tete na nyingi miongoni mwao zinaponea show za kiingilio kinywaji …hali ni hivyo hivyo pia kwa muziki wa dansi, bendi nyingi zinapumulia gesi huku bendi mbili tatu tu ndizo zinazofanya vizuri na kiingilio kinywaji kikibaki kuwa mkombozi wa bendi nyingi.
Kwa hali hiyo hutakosea ukisema hali si maridadi sana kwenye kumbi za starehe kwa bendi za taarab na dansi.
Sasa nije kwenye kile nilichokusudia kusema, ambacho kinaonekana kama kutia chumvi kwenye kidonda, hapa nazungumzia maonyesho maalum ya taarab au dansi ambayo kutokana nguvu kubwa zinazotumika kwenye matangazo, basi angalau kumbi hushamiri kwa mahudhudhirio yaliyonona, show hizi ni kama za uzinduzi wa bendi, uzinduzi wa albam, birthday za bendi, mpambano wa bendi mbili au zaidi, ujio wa wasanii wapya, ziara za mikoani na matukio mengine kadhaa ambayo angalau hutekenya hisia za mashabiki.
Huwa naumia sana matukio kama haya yanapogongana kwenye kumbi na siku zinazokaribiana na kusababisha kugawana wateja na wakati mwingine kusababisha hasara kubwa.
Labda nitoe mifano michache ili nieleweke zaidi. Tarehe 19 Disemba kulikwa na onyesho maalum la Mapacha Watatu na FM Academia pale Mzalendo Pub Kijitonyama, lakini siku hiyo hiyo Five Stars Modern Taarab nao pia walikuwa wanazindua albam ya mpya “Kichambo Kinakuhusu” ndani ya Travetine.
Kesho yake FM Academia, Mapacha Watatu na bendi nyingine mbili zikawa tena zina onyesho la pamoja Azura Beach Kawe, huku pale Mango Garden Kinondoni palitarajiwa kuwe na onyesho la miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta (kwa bahati mbaya likaahirishwa siku mbili kabla).
Travetine Hotel iliyokuwa na show ya Five Stars Disemba 19, ikawa pia na onyesho kubwa la Jahazi Modern Modern Taarab kutimiza miaka 8 Disemba 21, huku Disemba 26 kukiwa kuna show nyingine kubwa ya kutambulisha rasmi kundi la G5 Modern Taarab katika ukumbi huohuo.
Mjini Dodoma kutakuwa na Twanga Pepeta siku ya mkesha wa X-Mas, baada ya hapo kutakuwa na Msondo Ngoma Disemba 27, siku moja baada ya hapo watakuwepo FM Academia.
Wakazi wa Mbeya wataishuhudia Twanga Pepeta siku ya mkesha wa Mwaka Mpya, huku siku yenyewe ya mwaka mpya watakuwepo Malaika Band, lakini pia katika sherehe za X-Mas bendi za FM Academia na Rungwe Music Band ya kina Banza Stone, zitapishana mjini humo kwa siku moja tu.
Hiyo ni mifano michache tu ya ‘Kipwagu na Pwaguzi’ ya namna bendi za taarab na dansi zinavyoharibiana maonyesho yao aidha kwa makusudi, ubishi au kutojua.
Ipo haja ya makundi haya ya taarab na dansi, ambayo njia yao kuu ya mapato ni kiingilio cha ukumbini, kuwa na mtandao utakaodhibiti hali hii ambayo mwisho wa siku huongeza chuki pamoja na kufufua imani za kishirikina.
Chama cha muziki wa dansi (CHAMUDATA) kimelala usingizi wa pono na hakikubaliki miongoni wa wasanii kwa upande wa bendi za dansi, Chama cha Taarab nasikia nacho kiko chumba mahututi (ICU) kikipigania uhai, hali inayofanya muziki wa taarab na dansi uwe kama mifugo iliyotoroka zizini, kila mmoja na hamsini zake.

0 comments:
Post a Comment