MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo usiku wa jana amefunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 3-0 wa Real Madrid dhidi ya Celta Vigo Uwanja wa Bernabeu, Madrid.
Hiyo inakuwa hat-trick ya 23 kwa Mreno huyo na kwa ujumla anafikisha mabao 200 katika mechi 178 za La Liga tangu aanze kuichezea Real Madrid.
Aidha, mabao ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, aliyofunga dakika za 36 kwa penalti, 65 na 81 yanaifanya Real iendeleze wimbi lake la ushindi wa rekodi sasa, kwa mechi 18 mfululizo kwenye mashindano yote.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akibinuka tik tak katika mechi dhidi ya Celta Vigo jana, ambayo alifunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 3-0
Hata hivyo, katika mchezo huo, Real ilipata pigo baada ya mfungaji Bora wa Kombe la Dunia, James Rodriguez kutolewa nje kufuatia kuumia kipindi cha pili.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas; Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo; Rodriguez/Arbeloa dk53, Illarramendi, Kroos, Bale, Benzema/Coentrao dk81 na Ronaldo/Hernandez dk85.
Celta Vigo: Sergio; Mallo, Cabral/Gomez dk74, Fontas, Jonny, Radoja, Hernandez, Krohn-Dehli/Mina dk82, Orellana/Fernandez dk69, Nolito na Larrivey.
Cristiano Ronaldo akisherehekea hat trick yake Uwanja wa Bernabeu jana
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2863684/Real-Madrid-3-0-Celta-Vigo-Hat-trick-hero-Cristiano-Ronaldo-nets-200th-La-Liga-goal-extend-record-winning-run-18-games.html#ixzz3LBYmKEYH
0 comments:
Post a Comment