PAMBANO kubwa zaidi la ngumi kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao linaweza kufanyika Mashariki ya Kati.
Taarifa zimesema kwamba wawekezaji Falme za Kiarabu wametoa ofa ya Pauni Milioni 70 kusaidia maandalizi ya pambano hilo nchini Dubai.
Baada ya miaka ya kutambiana, inasemekana pambano babu kubwa lipo njiani kufanyika, Mei mwaka 2015 ikiwa ni tarehe inayotajwa kukubaliwa na mabondia wote wawili.
Manny Pacquiao akiwapungia mkono mashabiki mjini Manila baada ya kuwasili akitokea China ambako alimpiga Chris Algieri
Nyumbani kwa Mayweather, Las Vegas ni moja ya sehemu zinazopewa nafasi kubwa ya kufanyika pambano hilo, lakini mchezo wa mwisho wa Pacquiao ulifanyika Macau, China dhidi ya Chris Algieri na hiyo inatoa nafasi kwa pambano lake lijalo kufanyika sehemu nyingine.
Lakini Dubai inajitokeza kuwa sehemu nzuri ya tatu ya kufanyika kwa pambano hilo. Nchi hiyo ya Mashariki ya Kati haijawahi kuwa mwenyeji wa pambano kubwa la ngumu na tofauti ya muda kati ya Dubai na Marekani inaweza kuwa kigezo.
Pambano maarufu zaidi la Muhammad Ali na George Foreman lilifanyika Zaire (sasa DRC) miaka 40 iliyopita na Hasim Rahman alimpiga Lennox Lewis nchini Afrika Kusini mwaka 2001. Hivyo, inawezekana pambano kubwa la ngumu kufanyika nje ya Marekani.
Mayweather hajapoteza pambano hata moja baada ya kupigana mara 47
0 comments:
Post a Comment