MASHABIKI wa Barcelona wamepaza sauti kuonyesha namna wasivyoridhishwa na jezi mpya za msimu ujao za klabu hiyo zilizotambuliwa ambazo zitakuwa za ngazi ngazi badala ya mistari ya kushuka chini.
Katika miaka 115 ya historia klabu hiyo haijawahi kuvaa jezi za ngazi ngazi na mashabiki wa klabu hiyo ya Katalunya hawataki utamaduni huo uvunjwe.
Karika kura zilizopigwa kufanya maamuzi, asilimia 78 ya mashabiki wamesema hawapendi timu itumie jezi hizo mpya msimu ujao.
Lionel Messi akiwa amevalia jezi za asili za Barcelona miaka miatatu iliyopita
Henrik Larsson,Giovanni Van Bronckhorst, Carles Puyol, Ronaldinho na Xavi wakishangilia na jezi za asili za Barca miaka nane iliyopita
Romario akiifungia Barca katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Manchester United Uwanja wa Nou Camp msimu wa 1994-95
0 comments:
Post a Comment