RATIBA ya kusisimua ya Raundi ya Tatu ya Kombe la FA England imetolewa jana na Manchester United watasafiri kuwafuata ama Accrington au Yeovil, wakati Liverpool watamenyana na AFC Wimbledon, wakiwa na kumbukumbu ya fainali ya michuno huyo mwaka 1988 wakati Crazy Gang walipowakalisha mabingwa Uwanja wa Wembley.
Kutakuwa na mechi ya marudio ya timu zilizokutana msimu ulipita katika Fainali Wembley kati ya Arsenal na Hull, timu za Ligi Kuu England dhidi ya zisizo kwenye ligi na mechi nne za timu za Ligi Kuu tuou.
Lakini katika mechi 32, nyingi kati ya hizo zitasogezwa mbele kutoka Jumamosi, Januari 3 kutokana na wingi wa mechi za Ligi Kuu katika siku ya mwaka mpya.
Ratiba ya Raundi ya Tatu ya Kombe la FA imetolewa na ni ya kusisimua
0 comments:
Post a Comment