MABINGWA wa England, Manchester City kwa mara nyingine tena watamenyana na Barcelona katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya droo iliyopangwa mjini Nyon leo.
Tmu hiyo ya Katalunya, iliitoa timu ya Manuel Pellegrini katika hatua kama hiyo msimu uliopita kwa kipigo cha jumla cha mabao 4-1.
Chelsea itamenyana na mabingwa wa Ligue 1, Paris Saint-Germain- maana yake itakutana na beki wake wa zamani, David Luiz.
The Blues iliitoa timu hiyo ya Ufaransa katika Robo Fainali msimu uliopita kwa faida ya mabao ye ugenini, baada ya sare ya jujla ya 3-3, ikishinda 2-0 nyumbani na kufungwa 3-1 mjini Paris.
Wakati huo huo, Arsenal itamenyana na vigogo wengine wa Ufaransa, Monaco maana yake kocha Arsene Wenger atakitana na waajiri wake wa zamani.
0 comments:
Post a Comment