BONDIA Anthony Joshua anayetabiriwa kuwa Lennox Lewis mpya, amegoma kukubali ahadi ya kupewa fedha kwa hisani na mpinzani wake Kevin Johnson kuelekea pambano lao mwaka mpya.
Mmarekani huyo, ambaye hajapigwa katika mapambano yake 36, alitoa ofa ya kumpa asilimia 50 ya pato lake mpinzani wake huyo, Joshua iwapo atashinda.
Lakini Muingereza Joshua hakuwa tayari kukubali ofa hiyo katika Mkutano na Waandishi wa Habari.
Anthony Joshua na Kevin Johnson wakitunishiana vifua katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo
Wawili hao watapanda ulingoni kwenye ukumbi wa O2 mjini London Januari 31 ambalo linatarajiwa kuwa pambano gumu kwa Joshua tangu aanze kupigana ngumi za kulipwa.
Johnson alipigana na Vitali Klitschko mwaka 2009 na wote Dereck Chisora na Tyson Fury walishindwa kufurukuta mbele yake.
Johnson amesema: "Nataka kuweka makubaliano na yeye. Ikiwa Anthony atanipiga, nitachangia asilimia 50 ya pato langu kwake kwa hisani,".
Johnson na Joshua wakiwa wamepozi na promota Eddie Hearn katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini London
0 comments:
Post a Comment