VIGOGO Ivory Coast, Cameroon na Mali wamepangwa kundi moja, D Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mapema mwakani, wakati Zambia imepangwa Kundi B pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Cerpe Verde na Tunisia.
Afrika Kusini, au Bafana Bafana imejikuta katika kundi la vigogo kuelekea Fainali hizo za 2015 baada ya droo iliyopangwa leo usiku.
Vijana wa Shakes Mashaba wamewekwa Kundi C pamoja na Algeria na Ghana, ambao wote walikuwepo kwenye Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil. Timu nyingine katika kundi hilo ni Senegal.
Upangwaji wa makundi hayo ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Hicham El Amrani aliyesaidiwa na kiungo wa zamani wa kimataifa wa Misri, Mohamed Aboutreika, nyota wa zamani wa Cameroon aliyecheza Kombe la Dunia 1994 na 1998, Alphonse Tchami na kocha wa Afrika Kusini, Ephraim 'Shakes' Mashaba.
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 17 hadi Februari 8 Equatorial Guinea.
MAKUNDI YOTE AFCON 2015
Kundi A - Equatorial Guinea, Kongo, Gabon, Burkina Faso
Kundi B - Zambia, DRC, Cape Verde, Tunisia
Kundi C - Ghana, Senegal, Afrika Kusini, Algeria
Kundi D - Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea

0 comments:
Post a Comment