PAMOJA na kwamba ametangaza kurejea Arsenal siku moja, lakini gwiji wa The Gunners, Thierry Henry anaweza kuwahofia mashabiki wa timu yake ya zamani kutokana na kuvaa kofi ya wapinzani.
Henry, ambaye ametangaza kuondoka New York Red Bulls wiki hii, alibambwa akiwa amevaa kofia ya Spurs kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha Red Bulls.
Wakati kocha Arsene Wenger, ambaye amedokeza Henry anaweza kurudi Uwanja wa Emirates kama kocha, mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal hakuwahi kuwa mtu wa visasi kwa wapinzani wao wa Kaskazini mwa London, Tottenham.
Thierry Henry alikuwa amevalia kofia ya Spurs, lakini mashabiki wa Arsenal hawataki kumtilia shaka
Mfungaji huyo wa mabao ya rekodi Arsenal, alikuwa amevalia kofia ya timu ya mpira wa kikapu San Antonio Spurs inayocheza Ligi ya NBA, ambaye Henry anaishabiki.
Mfaransa huyo alipigwa picha hizo akiwa amevalia kofia hiyo wakati anawaaga wachezaji wenzake wa New York Red Bulls baada ya mechi yake ya mwisho.
Red Bulls ilifungwa mechi hiyo na New England Revolution mwishoni mwa wimi iliyopita na baada ya hapo, Henry akatangaza kuondoka.
Henry ni mfungaji bora wa kihistoria Arsenal, ambaye ameweka wazi nia yake ya kurejea katika klabu hiyo
0 comments:
Post a Comment