MSHAMBULIAJI Wayne Rooney yuko tayari kuichezea Manchester United katika mechi dhidi ya Southampton Jumatatu, baada ya kuukosa mchezo wa jana dhidi ya Stoke City kwa sababu ya majeruhi.
Inafahamika kwamba Rooney alisema mwenyewe yuko fiti juzi asubuhi baada ya kujiumiza mwenyewe kufuatia kujigonga kwenye bango la matangazo uwanjani katika mechi dhidi ya Hull City mwisho mwa wiki, lakini United ikaamua kupumzika katika mchezo wa Jumanne usiku.
Nahodha huyo wa United na England alifanyiwa vipimo leo na kuonekana kweli yuko fiti kabisa, hivyo anatarajiwa kurejea katika kikosi cha Louis van Gaal Uwanja wa St Mary’s.
Wayne Rooney atakuwepo kwenye mechi dhidi ya Southampton Jumatatu
0 comments:
Post a Comment