FIFA imesema Barcelona haitapewa ruhusa maalum ya kusajili beki baada ya kuumia kwa Thomas Vermaelen ambaye anatakiwa kuwa nje kwa miezi kadhaa.
Barcelona ilifikiri itapewa ruhusa maalum kwa mujibu wa sheria za Shirikisho la Soka Hispania licha ya kukabiliwa na adhabu ya mwaka mmoja ya FIFA kutosajili.
FIFA imeiambia Barcelona juzi kwamba Kamati yake ya Nidhamu haitoa ruhusa yoyote ya kusajili nje utaratibu wa kawaida wa usajili uliowekwa.
Thomas Vermaelen amekwenda kufanyiwa upasuaji ambao utamuweka nje kwa miezi kadhaa
FIFA iliifungia Barcelona kwa kuvunja sheria za kimataifa za usajili wa wachezaji wadogo. Itaanza Januari na itategemea na rufaa yao waliokata Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo.
Mbelgihi huyo aliyesajiliwa kutoka Arsenal kwa dau la Pauni Milioni 15 hajacheza tangu atue Camp Nou.
0 comments:
Post a Comment