TIMU ya Real Madrid imefungwa mabao 4-2 na AC Milan katika mchezo wa kirafiki Dubai uliochezwa katika mapumziko ya majira ya baridi.
Jeremy Menez aliifungia Milan bao la kwanza kabla dakika ya 24 ya Stephan El Shaarawy kuongeza la pili dakika ya 31.
Cristiano Ronaldo akaifungia la kwanza timu ya Carlo Ancelotti dakika 10 kabla ya mapumziko kabla ya El Shaarawy kufunga bao lake la pili katika mchezo huo dakika ya 49 na la tatu kwa Milan kipindi cha pili.
Giampaolo Pazzini aliyetokea benchi aligongeana vizuri na M'Baye Niang kuifungia Milan bao la nne dakika ya 72, kabla ya Karim Benzema kuifungia Real kwa penalti dakika sita kabla ya filimbi ya mwisho.
Nahodha wa AC Milan, Riccardo Montolivo akiwa ameiinua Kombe la Dubai Football Challenge baada ya kuifunga Real Madrid 4-2
Stephan El Shaarawy ameifungia AC Milan mabao mawili dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Real Madrid 4-2 katika mchezo wa kirafiki jana
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2891533/Real-Madrid-2-4-AC-Milan-Stephane-El-Shaarawy-scores-twice-Cristiano-Ronaldo-lose-time-September.html#ixzz3NSccfTWr
0 comments:
Post a Comment